Wednesday, January 7, 2015


kunasa tukio la aina yake baada ya kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Joni Simon kunaswa na kitita cha fedha bandia akitaka kuwekewa katika simu yake ya mkononi kupitia mtandao wa Tigo Pesa, tukio lililotokea Sinza Afrika Sana jijini Dar.


MKURUGENZI wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba wamewatolea uvivu mastaa wanaojihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya (mateja) na kuwataka waache wenyewe.

Monday, January 5, 2015


Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha za viongozi wa Panya Road kwa wanahabari.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu 510 wakiwemo viongozi watatu wa kundi linalojihusisha na uhalifu la ‘Panya Road’ .
Watu hao wamekamatwa katika operesheni inayoendeshwa na jeshi hilo, kupambana na uhalifu.



YULE mahabusu aliyeuawa kwa kupigwa risasi kwenye uzio wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Desemba 31, mwaka huu jijini Dar ni huyu ambaye anaonekana sura vizuri ukurasa wa kwanza wa gazeti hili.


MWALIMU Gaudencia Gitano (40) anayefundisha Shule ya Msingi Kivelu jijini Dar es Salaam, amedai huenda yeye ndiye anayeongoza kwa kupigwa kuliko wanawake wengine wote jijini, baada ya kudai anazo RB tano za vipigo tofauti kutoka kwa mumewe kwa nyakati mbalimbali tangu aolewe Oktoba 25, 2002, katika ndoa ya kiserikali iliyofungwa Ilala Boma.


WAKATI baadhi ya wasanii wa hapa jijini, Dar wakifa huzikwa hapahapa, jambo hilo limekuwa ni tofauti  kwa nyota wa filamu na muziki, Baby Madaha baada ya kufunguka kuwa akitokea amekufa hataki  kuzikwa Dar na badala yake azikiwe jijini, Mwanza.


MTANGAZAJI wa runinga Maimartha Jesse, ameweka wazi kuwa pamoja na watu kulalamika kuwa mwaka uliopita ulikuwa mgumu kifedha kwa upande wake amefanikisha kuingiza kiasi cha shilingi milioni 28 ambazo amezipata kupitia kazi zake za kila siku ikiwemo ya kundi lake maarufu la Baikoko.

Mrembo wa miss Universe Tanzania 2014,Carolyn Bernard ameondoka rasmi nchini kuelekea nchini Marekani kwenye fainali za  dunia za Miss Universe zitakazofanyika jijini Miami tarehe 25 mwezi huu wa januari.

Sunday, January 4, 2015



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
3 Januari, 2015



Fidel Odinga enzi za uhai wake.
MTOTO wa kwanza wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Fidel Odinga amefariki dunia leo alfajiri akiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya. Chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika. Raila Odinga amethibitisha kifo hicho.


Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa. Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta ikiwemo wenye daladala na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua.
Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.

ACHENI jamani! Vurugu tuzisikie tu kwa wenzetu! Kitendo cha vijana wachache wasio na maadili wanaojiita Panya Road kufanya fujo kidogo katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar, wakazi wa jiji hilo wamekitafsiri kitendo hicho na kusema Dar sasa si sehemu salama tena ya kuishi, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.


Makubwa! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke wa mtu aliyekuwa akiishi ukweni na mumewe wa ndoa, Bahati Ramadhani, amenusurika kuuawa na ndugu wa mumewe wakiwemo mawifi na wakwe zake baada ya kudaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko wake na kujikuta wakigombea mtoto.

                              Mwigizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel
LICHA ya kushauriwa na daktari kuhusu kutulia na kutovaa viatu virefu kutokana na ujauzito, mwigizaji Aunt Ezekiel ameonekana kuwa ni sikio la kufa kwani ameendelea kuvaa kama kawaida.Aunt aliendeleza ubishi huo Jumatano iliyopita mjini Dodoma alipokuwa amekwenda katika Pati ya Good Bye 2014 iliyoandaliwa na Kampuni ya Endless Fame ambapo mashabiki walimshuhudia Aunt akiwa amevaa kigauni kifupi pamoja na viatu virefu kama kawa.


Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akipozi.
Kumekuwa na maneno mengi juu ya nani mzuri kati ya staa wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’. Wema ametembea na Diamond na sasa Zari anadaiwa kuchukua uskani. Ijumaa Wikienda limechukua jukumu la kumaliza ubishi ambapo lilibandika swali hilo kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram, Facebook na Twitter. Maelfu ya mashabiki wao walipata nafasi ya kutoa ya moyoni. Majibu yaliyopatikana pima mwenyewe, ujiongeze.
Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO