Showing posts with label stars. Show all posts
Showing posts with label stars. Show all posts

Monday, April 13, 2015



Thursday, February 5, 2015


SIKU chache baada ya Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuweka picha zinazomuonesha mpenzi wake wa sasa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo.

Wednesday, January 7, 2015


INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au ‘waliamka’ nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh!

Monday, January 5, 2015



WAKATI baadhi ya wasanii wa hapa jijini, Dar wakifa huzikwa hapahapa, jambo hilo limekuwa ni tofauti  kwa nyota wa filamu na muziki, Baby Madaha baada ya kufunguka kuwa akitokea amekufa hataki  kuzikwa Dar na badala yake azikiwe jijini, Mwanza.


MTANGAZAJI wa runinga Maimartha Jesse, ameweka wazi kuwa pamoja na watu kulalamika kuwa mwaka uliopita ulikuwa mgumu kifedha kwa upande wake amefanikisha kuingiza kiasi cha shilingi milioni 28 ambazo amezipata kupitia kazi zake za kila siku ikiwemo ya kundi lake maarufu la Baikoko.

Sunday, January 4, 2015


                              Mwigizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel
LICHA ya kushauriwa na daktari kuhusu kutulia na kutovaa viatu virefu kutokana na ujauzito, mwigizaji Aunt Ezekiel ameonekana kuwa ni sikio la kufa kwani ameendelea kuvaa kama kawaida.Aunt aliendeleza ubishi huo Jumatano iliyopita mjini Dodoma alipokuwa amekwenda katika Pati ya Good Bye 2014 iliyoandaliwa na Kampuni ya Endless Fame ambapo mashabiki walimshuhudia Aunt akiwa amevaa kigauni kifupi pamoja na viatu virefu kama kawa.


Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akipozi.
Kumekuwa na maneno mengi juu ya nani mzuri kati ya staa wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’. Wema ametembea na Diamond na sasa Zari anadaiwa kuchukua uskani. Ijumaa Wikienda limechukua jukumu la kumaliza ubishi ambapo lilibandika swali hilo kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram, Facebook na Twitter. Maelfu ya mashabiki wao walipata nafasi ya kutoa ya moyoni. Majibu yaliyopatikana pima mwenyewe, ujiongeze.

Tuesday, December 30, 2014


BAADA ya wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kwenye moja ya magazeti pendwa kuwa hana uhusiano na mtu yeyote ndani ya Bongo Muvi na yupo mbioni kumuanika mrithi wa Sajuki mengi yameendelea kuibuka.

Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Rwanda jana.

Tuesday, December 23, 2014





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul  'Diamond Platnumz' baada ya kumtembelea leo Ikulu jijini Dar es Salaam.



KIFO cha utata cha mnenguaji nyota Bongo, Mwanaisha Mbegu maarufu kama Aisha Madinda, kimemuibua Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ wa FM Academia, aliyewataka wenzake kuwa makini ili kutojiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya.
Akistorisha na paparazi wetu, Queen Suzy alisema ameumizwa sana na kifo hicho kwani ameacha pengo kubwa kutokana na unenguaji wake mzuri, huku chanzo cha kifo chake kikiwa hakifahamiki sawasawa.
“Nawasihi wanenguaji wenzangu na wanamuziki wote, tusidanganyike kuingia kwenye vishawishi vya matumizi ya madawa ya kulevya, maana mfano Aisha alikuwa mzuri kweli kwenye kazi, lakini alipojiingiza kwenye unga kiwango chake kikashuka sana,” alisema Queen Suzy.


MASTAA wa filamu Bongo, Nisha, Odama na Aunt Ezekiel wameipongeza kampuni ya Steps Entertainments kwa kitendo chake cha kuagiza mtambo wa kurekodia filamu kitu ambacho kitawasaidia wasanii kufaidika.
“Kitendo cha kurekodia nje ya nchi kilikuwa kinawafanya wasambazaji kuongeza gharama za filamu zetu kwa walaji, kitu ambacho kilikuwa kikiwafanya wanakimbilia kwa wezi wa kazi zetu kwa sababu ya urahisi wa bei, lakini wao kwa kuleta mtambo huo, ina maana filamu zitashuka bei na zikiwa na ubora, ni jambo zuri sana,” alisema Odama akiwa pamoja na wenzake hao.

Sir Elton John akikata keki na mpenzi wake David Furnish.

Monday, December 22, 2014


WIKI iliyopita tuliishia pale ambapo staa wa Bongo Fleva, Diamond aliachia video yake ya Number One katika uzinduzi usiyo na kiingilio alioufanya ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo pia alimzawadia gari, aliyekuwa mwanamuziki nguli nchini, marehemu Muhidin Maalim Gurumo.
Wiki hii tunaendelea ambapo katika kuanika maisha yake, Diamond anasema:

Sunday, December 21, 2014




STAA wa filamu Bongo ambaye miezi michache iliyopita alifunga pingu za maisha na mwanaume mwenye asili ya Denmark, Lucy Komba amekwea pipa kuelekea nchini humo kwenda kuishi na mumewe sambamba na kumpelekea mwanaye amlee.


STAA wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema anakumbuka fadhila za marehemu Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ ndiyo maana amejitoa kwa hali na mali katika msiba wake kwani anawaonea huruma watoto wake ambao aliishi nao kama kaka yao enzi za marehemu alipokuwa na uhusiano na mdau wa Muziki wa Dansi Bongo, Fikiri Madinda.


WAKATI kila mtu akiamini mwalimu wake wa lugha ya Kiingereza ni Wema Sepetu ‘Madam’ staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kudai aliyemfundisha lugha hiyo ni aliyekuwa mpenzi wake, Peniel Mungilwa‘Diamond aliwataka watu wote waliokuwa wakiamini Wema ndiye mwalimu wake wa ung’eng’e wafute imani hiyo kwani Penny ndiye mpango mzima.

Thursday, December 18, 2014




Ijumaa: Umekuwa ukitajwa kuwa wewe ni msanii wa kike unayeongoza kwa kubadilisha mabwana kila kukicha, hili likoje?
Baby Madaha: Ukweli hiyo huwa inatokea tu na huwa sipendi kusumbuliwa na mwanaume, nikiona ananizingua nammwaga. Hata hivyo, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza, nafanya kazi, mapenzi pembeni.
Ijumaa: Unadhani kwa nini umekuwa ukiingia kwenye uhusiano kisha kutoswa, ni umachepele wako au kitu gani?


Mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' (wa tatu kulia) akipata chakula cha usiku na wageni wake wakiongozwa na staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' (katikati) usiku wa kuamkia leo nchini Uganda.


Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Uganda jana.
Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO