Showing posts with label TZ. Show all posts
Showing posts with label TZ. Show all posts

Monday, April 13, 2015



Tuesday, March 24, 2015



Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud akizungumza na wanahabari.

Wednesday, March 11, 2015



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing alipofika Ikulu Mjini Zanzibar (kulia) Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Xie Yunliang.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na mgeni wake Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.[Picha na Ikulu.]

Friday, February 20, 2015



MWAKILISHI Mkazi wa Shirika la JICA nchini Tanzania, Onishi Yasunora akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesm Mramba (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa kuzungumzia maendeleo ya miradi ya kuboresha na kukarabati miundombinu ya umeme hapa nchini. Mkutno huo ulifanyika Dar es Salaam. Pamoja nao ni Waziri pia mkuu wa Kazi wa Ubalozi wa Japan hapa Nchini, Kazuyoshi Matsunaga.


 Jeneza lenye Mwili wa marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari kushushwa nyumbani kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na kutoa heshima za mwisho zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili wake katika Nyumba yake ya Milele.

Monday, January 26, 2015


Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo ya mradi wa nyumba za kuuza za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli na Msimamizi wa mradi huo Bw. Hassan Bendera.

Naibu waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akikabidhiwa ua na mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Christina Nyenga wakati wa mapokezi ya Naibu Waziri jijini Dar es Salaam.

Thursday, January 22, 2015



INATOSHA! Mrembo, Happiness Wilfred Nassari (27), ameibuka na kudai kuwa amekuwa akisali bila nguo kwenye ibada ya imani ya Freemason inayosifika kwa ushirikina.


NYUMA ya ukaribu wa Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, kuna siri nzito kufuatia mambo mbalimbali yanayojitokeza kati yao kila kukicha, Amani lina cha kukujuza.

Tuesday, January 13, 2015

http://api.ning.com/files/lET3ABatHUmDiD-UbGbBA0lWqrPXqrAST2WNxFCIn-GIknHxO3g2WW4YmetIJa5S9xLlruUYL8BBcDdsDgwaiEVbeMgjvFIW/ScreenShot20150113at2.47.42PM.png

Friday, January 9, 2015



Msanii wa bendi anayefanya vizuri, Christian Bella (kushoto)  na Mama Kanumba wakionyesha kitabu hicho kwa wanahabari (hawapo pichani).

DSC_0002
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
Na mwandishi wetu, Shinyanga
MKUU wa wilaya ya Shinyanga AnneRose Nyamubi ameomba jamii ya watanzania kusaidia kupatikana kwa zahanati katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Buhangija ili kupunguza adha wanazopata watoto hao katika huduma za afya.
Kauli hiyo ameitoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika kituo hicho akiambatana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukiongozwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Nyamubi amesema kwamba ingawa hospitali ya mkoa ina dirisha kwa ajili ya matibabu ya watoto hao,wakati mwingine inakuwa shida daktari maalumu anayehusika anapokuwa hayupo.
Aidha alisema kwa namna watoto hao walivyo wanahitaji huduma ya karibu ya kitiba ambayo inawezekana kama kituo hicho kingekuwa na zahanati yake.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Desemba, 2014 leo jijini Dar es salaam.Wengine ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja (kushoto) na Johnson Nyella, Meneja Utafiti wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).


Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Mh. Lennarth Hjelmaker akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza, Rakesh Rajani iliyofanyika jana jioni kwenye viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, wakiwa katika Sala na Dua ya kumuombea aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali kabla ya mazishi yake iliyofanyika Januari 08,2015 katika msikiti wa Mohammed Ali Jang’ombe Zanzibar.

Wednesday, January 7, 2015



Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kwenye Ofisi ya Mtendaji  kata ya Mlimani Katika Mfululizo wa Ziara zake katika Kata mbalimbali Jimbo la Morogoro mjini.

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyakazi wastaafu Pemba Bwana Majid Moh’d akimkabidhi risala Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya hiyo hapo ukumbi wa Tasaf Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Chake chake Pemba.
DSC_0495


SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista Germaine Baibika akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
Alisema jumla ya mabinti 634 wamehitimu mafunzo ya miezi miwili yanayogusa haki za binadamu, haki zao, masuala ya afya na kuzitambua na kuezinzi mila nzuri.
Aidha wamejifunza kazi za sanaa na usanii.
Alisema adha kubwa wanayokumbana nayo mabinti hao waliotoka katika kituo hicho ni kukamatwa kwa nguvu na kupitishwa kisu cha Ngariba bila wao wenyewe kuafiki kwa dai la kuendeleza mila.
“Hii sio mila” anasema sista Germaine na kuongeza kuwa hakuna mila inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au kulazimisha mambo yasiyofaa katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima ipigwe vita.
Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO