MWISHONI mwa wiki kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania iliibuka
kinara wa pili kwa walipa kodi wakubwa na inaongoza katika kundi la
sekta ya mawasiliano nchini ambapo haijawahi kutokea.
Akiongea katika kilele cha maadhimisho ya 8 ya Wiki ya Mlipa Kodi
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere,
Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania,Richard Kayombo, aliyataja makampuni 3 yanayoongoza kwa kufuata
kanuni bora za ulipaji kodi na utunzaji wa kumbukumbu za kulipa kodi
nchini kuwa ni Kampuni ya Bia Tanzania, Kampuni ya Vodacom na Kampuni ya
kutengeneza sigara.
Akiongea muda mfupi baada ya kutunukiwa kikombe na cheti cha ushindi
kutoka kwa mgeni wa heshima ambaye alikuwa ni Waziri Kiongozi mstaafu wa
Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania Kelvin Twisa alisema “Napenda kuishukuru Serikali kwa kutambua
mchango wetu wa kuchangia mapato na vilevile nawashukuru wafanyakazi
wote wa Vodacom na wateja wote ambao wanaendelea kutuweka mbele kwa
ushirikiano wao na kutuamini ambapo tumeweza kuwa wachangiaji wakubwa.