MWISHONI mwa wiki kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania iliibuka kinara wa pili kwa walipa kodi wakubwa na inaongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano nchini ambapo haijawahi kutokea.
Akiongea katika kilele cha maadhimisho ya 8 ya Wiki ya Mlipa Kodi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania,Richard Kayombo, aliyataja makampuni 3 yanayoongoza kwa kufuata kanuni bora za ulipaji kodi na utunzaji wa kumbukumbu za kulipa kodi nchini kuwa ni Kampuni ya Bia Tanzania, Kampuni ya Vodacom na Kampuni ya kutengeneza sigara.
Akiongea muda mfupi baada ya kutunukiwa kikombe na cheti cha ushindi kutoka kwa mgeni wa heshima ambaye alikuwa ni Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twisa alisema “Napenda kuishukuru Serikali kwa kutambua mchango wetu wa kuchangia mapato na vilevile nawashukuru wafanyakazi wote wa Vodacom na wateja wote ambao wanaendelea kutuweka mbele kwa ushirikiano wao na kutuamini ambapo tumeweza kuwa wachangiaji wakubwa.
0 comments:
Post a Comment