TIMU ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la
Mbeya, imetangaza kujiondoa rasmi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu
Bara msimu huu baada ya kuanza vibaya kwenye mechi saba na akili zote
sasa wamezielekeza katika kuiokoa timu hiyo na janga la kushuka daraja.