Friday, April 10, 2015



Waziri wa kazi na ajira mhe.Gaudencia Kabaka
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)

Pia  Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.
Yaliokuwa malalamiko ya madereva  ilikuwa ni pamoja na kukerwa na tochi za barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.
Na serikali imetoa agizo Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na askari wa usalama barabarani  wameagizwa kulifatilia hilo.

0 comments:

Post a Comment

Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO