Tuesday, November 18, 2014

Staa wa filamu za kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’.
STAA wa filamu za kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ambaye aliripotiwa kuondoka katika kundi maarufu la Bongo Movie Unity, anadaiwa kutaka kurejea kundini baada ya kuona anakosa madili.



Chanzo kilicho karibu na msanii huyo kimesema maisha mazuri aliyokuwa akiishi ndani ya kundi hilo, kwa kupata mishemishe za kila mara, ndizo hasa zinazomfanya atake kurejea.
Lakini nyota huyo alipozungumza na gazeti hili, alishangazwa na habari hizo na kudai kuwa anasikia juu ya suala hilo, lakini siyo  kweli, kwani pamoja na ukweli kwamba yeye aligombana na mtu mmoja tu Bongo Movie, bado hawezi kutaka kurudi kwa vile yeye kama mjasiriamali, ana vitu vingi vya kufanya.

0 comments:

Post a Comment

Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO