Wednesday, January 7, 2015


Katibu wa Jumuiya ya Wafanyakazi wastaafu Pemba Bwana Majid Moh’d akimkabidhi risala Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya hiyo hapo ukumbi wa Tasaf Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Chake chake Pemba.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Wafanyakazi Wastaafu Pemba akifuatilia Hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akiizindua rasmi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiizindua rasmi Bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Wafanyakazi Wastaafu Pemba hapo ukumbi wa Tasaf uliopo Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Chake chake Pemba.
Wastaafu wa Taasisi za Umma za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na zile za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanapaswa  kushirikiana kwa karibu katika kutumia ujuzi na Taaluma zao za muda mrefu ndani ya Jumuiya wanazozianzisha baada ya kustaafu kwao  ili waendelee kuchangia Maendeleo ya Taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiizindua rasmi Bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Wastaafu Pemba hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Tasaf  uliopo katika Majengo ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar yaliyopo Chake chake Pemba.
Balozi Seif alisema mashirikiano hayo yatatoa nafasi nzuri kwa wastaafu hao kuondoa shaka ya kuendeleza maisha yao kwani baadhi yao hupata wakati mgumu  kabla na baada ya kustaafu kwa vile wanakuwa bado hawajajipanga.

0 comments:

Post a Comment

Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO