Thursday, January 29, 2015


Michelle Obama (wa pili kushoto) anaonekana hana raha wakati akiwa Saudi Arabia na mumewe, Rais Obama, wakati walipokwenda kuomboleza msiba wa Mfalme Abdullah.

Michelle akiwa na sura iliyokosa uchangamfu na tabasamu.
Ujumbe wa Obama ulipokutana na Mfalme Salman (wa pili kulia) wa Saudi Arabia.
MICHELLE OBAMA, mke wa Rais wa Marekani, ambaye alikuwa ziarani juzi nchini Saudia hakuonekana na uso wa furaha wakati yeye na mumewe walipokwenda nchini humo kuhani msiba wa Mfalme Abdullah aliyefariki dunia hivi karibuni.
Baada ya kuondoka mjini New Delhi walipokuwa na ziara rasmi,Michelle alibadili nguo zake na kuvaa nguo ndefu tangu kwenye mikono hadi chini.  Lakini, katika kukutana na kusalimiana na viongozi wa nchini humo, akiwemo mfalme mpya,  Salman, wengi wao walikataa kushikana mikono na mama huyo, kwa imani za kidini na pengine kwa kuwa alikuwa hajajistiri kichwani kwa kuvaa hijabu.
Nchini Saudi Arabia, wanawake hawaruhusiwi kutembea ‘kichwa wazi’ na wanabanwa na masharti mengi ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kuendesha gari, kutofungua akaunti benki bila ya kibali cha mume, kutotembea ‘mitaani’ bila kuwa na mume au mwenza, kutojaribia nguo madukani wakati wa kuzinunua, na mambo mengine yanayozingatia mila za nchi hiyo.
Matokeo yake, mama huyo alijikuta hana furaha wakati wa ziara hiyo kutokana na msimamo wake wa kuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanawake duniani.

0 comments:

Post a Comment

Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO