
MTANGAZAJI wa runinga Maimartha Jesse, ameweka wazi kuwa pamoja na watu kulalamika kuwa mwaka uliopita ulikuwa mgumu kifedha kwa upande wake amefanikisha kuingiza kiasi cha shilingi milioni 28 ambazo amezipata kupitia kazi zake za kila siku ikiwemo ya kundi lake maarufu la Baikoko.

“Nimepata pesa nyingi maana kama ningekaa tu nyumbani nisingeweza kupata hata hizo milioni 28, namshukuru Mungu kwa sababu nimeweza kufanya kazi zangu kwa ubora na kupata kiasi hicho, lakini kifupi ni kwamba sijafanya dili feki za kupata pesa,” alisema Maimartha.
0 comments:
Post a Comment