
Damu na makaratasi vikiwa vimetapakaa kila mahali katika ofisi za jarida la Charlie Hebdo baada ya kuvamiwa na magaidi.


za jarida la Charlie Hebdo baada ya kuvamiwa na magaidi.


Uchunguzi wa shambulio hilo ukiendelea mitaani.

wakati wanatoka kufanya mauaji katika ofisi za jarida hilo.
Mmoja wa magaidi (chini kulia) akitokomea baada ya kumuua polisi.
PICHA za mwanzo zimetolewa kuonyesha hali ilivyokuwa
katika uvamizi wa ofisi za jarida la vikatuni la Charlie Hebdo jijini
Paris, Ufaransa, Jumatano wiki hii ambapo magaidi wawili waliwaua watu
12 na kujeruhi saba.
Magaidi hao wanasemekana walivamia ofisi hizo kutokana na chuki za kutoa vibonzo vyenye kuukashifu Uislam ikiwa ni pamoja na kuchapisha vikatuni vya kumkejeli Mtume Muhammad.
Katika msako mkali unaoendelea nchini Ufaransa, hadi sasa watuhumiwa watatu wamekamatwa kuhusika na shambulio hilo ambao ni Saidi Kouachi (34) na ndugu yake, Cherif Kouachi (32), ambapo Hamyd Mourad (18) kutoka Reims nchini Ufaransa, alijisalimisha mwenyewe baada ya kugundua anatafutwa na polisi.
0 comments:
Post a Comment