Jeneza
lenye Mwili wa marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari
kushushwa nyumbani kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na
kutoa heshima za mwisho zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili
wake katika Nyumba yake ya Milele.
Askari wa Jeshi la Polisi
Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa DCP Mstaafu wa
Jeshi la Polisi Tanzania Mzee Andrew Michael Kumalilwa wakiingia
katika nyumba yake iliyopo Tabata Segerea kwaajili ya Misa na ndugu,
jamaa na marafiki kutoa heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha
katika Nyumba yake ya Milele ambapo Marehemu alizikwa katika nyumba
kwake Tabata Segerea.
Mtoto
wa Kwanza wa Marehemu Andrew Michael Kumalilwa, Patricia Andrew akiwa
mwenye huzuni wakati wa msiba wa marehemu Baba yake ambapo marehemu
alikuwa mstaafu wa jeshi la Polisi Tanzania akiwa na Cheo cha DCP.
Jeneza lililokuwa
limebeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukitolewa
katika chumba cha kuhifadhia maiti kwaajili ya kuelekea nyumbani Kwake
Segerea ambapo mazishi yalifanyika
0 comments:
Post a Comment