Gazeti la Vibonzo la Charlie Hebdo.
Gazeti la kila wiki la vibonzo la Charlie Hebdo la Ufaransa toleo la
kesho Jumatano linatarajiwa kuchapisha kibonzo cha Mtume Muhammad katika
ukurasa wake wa mbele chini ya kichwa cha habari "Yote yameshasamehewa"Tuesday, January 13, 2015
Friday, January 9, 2015
5:13 AM
Hon.Cisko
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi mara
baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya
kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo
walemavu wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
Na mwandishi wetu, ShinyangaMKUU wa wilaya ya Shinyanga AnneRose Nyamubi ameomba jamii ya watanzania kusaidia kupatikana kwa zahanati katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Buhangija ili kupunguza adha wanazopata watoto hao katika huduma za afya.
Kauli hiyo ameitoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika kituo hicho akiambatana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukiongozwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Nyamubi amesema kwamba ingawa hospitali ya mkoa ina dirisha kwa ajili ya matibabu ya watoto hao,wakati mwingine inakuwa shida daktari maalumu anayehusika anapokuwa hayupo.
Aidha alisema kwa namna watoto hao walivyo wanahitaji huduma ya karibu ya kitiba ambayo inawezekana kama kituo hicho kingekuwa na zahanati yake.
5:05 AM
Hon.Cisko
Mkurugenzi
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw.
Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kupungua kwa mfumuko wa bei nchini
kwa mwezi Desemba, 2014 leo jijini Dar es salaam.Wengine ni Meneja wa
Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja (kushoto) na
Johnson Nyella, Meneja Utafiti wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
5:00 AM
Hon.Cisko
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, wakiwa katika Sala na Dua ya kumuombea aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali kabla ya mazishi yake iliyofanyika Januari 08,2015 katika msikiti wa Mohammed Ali Jang’ombe Zanzibar.
Wednesday, January 7, 2015
3:59 AM
Hon.Cisko
Katibu
wa Jumuiya ya Wafanyakazi wastaafu Pemba Bwana Majid Moh’d akimkabidhi
risala Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye
hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya hiyo hapo ukumbi wa
Tasaf Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Chake chake Pemba.
3:50 AM
Hon.Cisko
SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista Germaine Baibika akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
Alisema jumla ya mabinti 634 wamehitimu mafunzo ya miezi miwili yanayogusa haki za binadamu, haki zao, masuala ya afya na kuzitambua na kuezinzi mila nzuri.
Aidha wamejifunza kazi za sanaa na usanii.
Alisema adha kubwa wanayokumbana nayo mabinti hao waliotoka katika kituo hicho ni kukamatwa kwa nguvu na kupitishwa kisu cha Ngariba bila wao wenyewe kuafiki kwa dai la kuendeleza mila.
“Hii sio mila” anasema sista Germaine na kuongeza kuwa hakuna mila inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au kulazimisha mambo yasiyofaa katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima ipigwe vita.
Subscribe to:
Posts (Atom)
RSS Feed
Twitter
