Friday, February 20, 2015



MWAKILISHI Mkazi wa Shirika la JICA nchini Tanzania, Onishi Yasunora akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesm Mramba (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa kuzungumzia maendeleo ya miradi ya kuboresha na kukarabati miundombinu ya umeme hapa nchini. Mkutno huo ulifanyika Dar es Salaam. Pamoja nao ni Waziri pia mkuu wa Kazi wa Ubalozi wa Japan hapa Nchini, Kazuyoshi Matsunaga.

Askari polisi wa doria ya pikipiki maarufu kama tigo wakiongea  na kijana aliyekuwa akiendesha pikipiki na mtu aliyempakiza.


 Jeneza lenye Mwili wa marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari kushushwa nyumbani kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na kutoa heshima za mwisho zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili wake katika Nyumba yake ya Milele.

Kikundi cha wasanii mkoani Dodoma, kikitoa burudani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, mjini Dodoma. Mkutano huo umemalizika leo Alhamisi Feb 19, 2015




 Mshauri mkuu wa mradi wa NewsRadar, Romana Gersuni kutoka Ujerumani akielezea jinsi teknolojia hiyo mpya na ya kisasa ya ukusanyaji taarifa mbalimbali ya Push Observer inavyofanyakazi zake.

Friday, February 13, 2015




Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Abdulkarim Esmail Hassan Shah (Mafia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki na kuambatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Tumaini Thika jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.

Wednesday, February 11, 2015




Mkurugenzi wa masoko wa Airtel bw. Levi Nyakundi (kushoto) akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Yatosha Zaidi bi. Mwajabu Omary leo katika makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Tanzania. Anayeshuhudia (katikati) Mkurugenzi wa wa kitengo cha Mawasiliano bi Beatrice Singano Mallaya .Airtel imekabidhi magari matatu katika hafla hiyo.

Mwendesha bodaboda akiendelea kuteketea kwa moto baada ya kuchomwa na wananchi wenye hasira katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam,  juzi jioni ambapo alidaiwa kumpora mkoba dada mmoja na kujaribu kukimbia.

Tuesday, February 10, 2015



KIMENUKA! Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito shemeji wa Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana kwa kitendo cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.

Thursday, February 5, 2015


SIKU chache baada ya Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuweka picha zinazomuonesha mpenzi wake wa sasa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo.
Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO