Tuesday, December 30, 2014

Mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude Rwakatare (pichani) ameibuka na kusema hafikirii kugombea nafasi hiyo mwakani.

BAADA ya wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kwenye moja ya magazeti pendwa kuwa hana uhusiano na mtu yeyote ndani ya Bongo Muvi na yupo mbioni kumuanika mrithi wa Sajuki mengi yameendelea kuibuka.

IKIWA  imebakia siku moja kabla ya mwaka 2014 kumalizika, jiji la Dar es Salaam limejikuta likigubikwa na mauaji ya mara kwa mara, hasa ya kutumia silaha baada ya kubainika kuzagaa kwa bastola zilizo mikononi mwa watu waovu.

MENGI yameibuka kufuatia waimba Injili Bongo kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo ndoa zao kuvunjika, madai ya kuchepuka, kupata ujauzito nje ya ndoa na matumizi ya madawa ya kulevya, Uwazi limechimba na kuchimbua.
angalia hapa..........

Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Rwanda jana.

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri.

Tuesday, December 23, 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul  'Diamond Platnumz' baada ya kumtembelea leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Eliakim Maswi.

MAAJABU! Ndivyo unavyoweza kusema unapokutana na mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina  la Frank Kalamu (53) mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam, aliyetoa ushuhuda wa kufunga mwaka kwamba kwa zaidi ya miaka miwili, alikuwa akipata siku zake kama ilivyo kwa wanawake, ingawa yeye ni kupitia njia ya haja kubwa.

Mapenzi bhana! Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia kwenye ‘utamu’ wa penzi la mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika siri tano za kilichomvutia kwa staa huyo gumzo Afrika Mashariki.

KIFO cha utata cha mnenguaji nyota Bongo, Mwanaisha Mbegu maarufu kama Aisha Madinda, kimemuibua Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ wa FM Academia, aliyewataka wenzake kuwa makini ili kutojiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya.
Akistorisha na paparazi wetu, Queen Suzy alisema ameumizwa sana na kifo hicho kwani ameacha pengo kubwa kutokana na unenguaji wake mzuri, huku chanzo cha kifo chake kikiwa hakifahamiki sawasawa.
“Nawasihi wanenguaji wenzangu na wanamuziki wote, tusidanganyike kuingia kwenye vishawishi vya matumizi ya madawa ya kulevya, maana mfano Aisha alikuwa mzuri kweli kwenye kazi, lakini alipojiingiza kwenye unga kiwango chake kikashuka sana,” alisema Queen Suzy.

MWANAMITINDO anayefanya vizuri katika urembo ambaye hivi karibuni aliingia mkataba wa mabilioni na kampuni ya Rainbow Shell ya China, Jokate Mwegelo amesema katika harakati zake za kusaka mafanikio, hajawahi kukanyaga kwa waganga zaidi ya kumtegemea Mungu pekee.
Jokate ambaye brand yake inakwenda kwa jina la Kidoti alisema; “Ninatumia akili yangu pamoja na watu wangu kutoka crew yangu hadi hatua tuliyofikia, mambo yakiwa magumu namlilia Mungu kwa kusali kila siku kwa imani yangu huwa naamini naweza kushinda bila kwenda kwa mganga.”

MASTAA wa filamu Bongo, Nisha, Odama na Aunt Ezekiel wameipongeza kampuni ya Steps Entertainments kwa kitendo chake cha kuagiza mtambo wa kurekodia filamu kitu ambacho kitawasaidia wasanii kufaidika.
“Kitendo cha kurekodia nje ya nchi kilikuwa kinawafanya wasambazaji kuongeza gharama za filamu zetu kwa walaji, kitu ambacho kilikuwa kikiwafanya wanakimbilia kwa wezi wa kazi zetu kwa sababu ya urahisi wa bei, lakini wao kwa kuleta mtambo huo, ina maana filamu zitashuka bei na zikiwa na ubora, ni jambo zuri sana,” alisema Odama akiwa pamoja na wenzake hao.

MBUNGE wa Sengerema (CCM), William Ngeleja ameweka wazi kuwa pamoja na ushindani kuwa mkubwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni, anajivunia ushindi mzito walioupata kupitia chama chake.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameleta hoja ya kujadili ndani ya kaya yangu ‘alipojisheheresha’ kuwa yeye ni jembe kwa mkuu mwenzangu wa kaya yaani Rais Jakaya Kikwete, hii ni kauli ya hivi majuzi tu.

Sir Elton John akikata keki na mpenzi wake David Furnish.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo Desemba 22, 2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia.
--Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya maadili pia wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Tibaijuka.
--Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Tibaijuka, tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine.
--Mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Fredreck Werema ameshajiuzulu na amesema amebeba dhamana hiyo pia kwa niaba ya waliojiuzulu.
--Kuhusu watu kuwawajibisha, bodi ya TANESCO bahati nzuri imemaliza muda wake na tumeanza mchakato wa bodi, na tutaipata siku chache zijazo. Katibu mkuu wa wizara ni mtumishi wa umma, hivyo kuna taratibu na nimeshaagiza zianze.
----Serikali iandae muswada wa sheria ulioleta TAKUKURU, ni wazo zuri, Mchakato wa kufanya mageuzi TAKUKURU tumeuanza tangu 2008. Sheria ya kwanza ya PCCB ilikua na makosa manne tu ya rushwa tukayaongeza mpaka 24.
--Kuhusu mabenki kuwekwa kama zinatakatisha fedha, pendekezo uchunguzi ufanyike ni pendekezo zuri na intelligence unit ndio watakaofatilia
--Rais aunde tume ya kijaji kuwachunguza majaji(Mujulizi na Luangisa), nimelipokea lakini utaratibu wa kisheria kushughulikia linatakiwa lianzie kwenye mahakama na sio linaanzia kwa rais au bunge. Mahakama inaporidhika amepoteza sifa, inaletwa kwa rais maana ndie anaeteua majaji. Lazima kushirikiana na muhumili wenyewe. Nilichosema tumwachie jaji mkuu na wakiridhika watakuja kwa raisi endapo wataridhika wahusika wamekosa sifa.
--Kamati za bunge kuwavua nyadhifa wenyeviti wa kamati za bunge tunaliachia bunge lenyewe
--TAKUKURU na jeshi la usalama vichukue hatua, nimeshaeleza hatua zinaendelea.
--Kuhusu uwazi wa mikataba na mapitio, tutafanya na lipo moja tutafanya kuhusu usiri wao wa biashara, kuweka wazi zinaweza kutumiwa na wapinzani wa kibiashara, hivyo tutaangalia namna ya kulifanya.
--Niwahakikishie mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira katika kutimiza maazimio ya bunge.
Kutaifisha mitambo ya IPTL, tunahimiza sekta binafsi kuwekeza, tunapotaifisha habari tunayopeleka si nzuri, sisi tuliotaifisha mwanzo siku hizi tunasema hatuna sera ya ujamaa hivyo waje kuwekeza. Watasema wale jamaa wamerudia tena wanataifisha. Mahakama imefanya maamuzi kwa IPTL, kwanza waibadili mitambo yao ibadili itumie gas badala ya mafuta, tukiyafatilia yanaweza kutufikisha mahali. Haya ya kutaifisha yananipa wasiwasi

--Maazimio ya bunge
Kwanza niseme serikali imayakubali na niwapongeze waheshimiwa wabunge. Nashukuru kamati ya bunge chini ya Zitto na Filikunjombe, watu wa upinzani kufanya yale maamuzi yao, kwamba CCM ni mafisadi. Ni kweli watu hawa wanatoka CCM ila sio kwamba CCM inaridhia. Ntashangaa mbunge kulipinga hili eti kisa tu yuko CCM, bunge wengi ni CCM, kama ni kweli walikuwa hawataki hakuna azimio lingepita? Na kuna baadhi ya wabunge wa CCM waliudhika na maovu haya, wenzetu wanatafuta sifa laini kwa jambo ambalo ni letu sote.

--VIP walipouza na kupata dola milioni 78, wamelipa kodi bilioni 38. Kulikua na tuhuma za rushwa katika mchakato mzima. Yamesemwa mengi na bado hatujamaliza kuyasoma, rushwa ni kosa la jinai. Nilielekeza taarifa walizozipata wazipeleke PCCB. Nimeambiwa wanaendelea na mchakato wao. Kwa miamala, serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa mujibu wa taratibu, maaskofu na masheikh kupewa kitu hawatuhusu, mtumishi wa umma ana masharti ya kupokea fedha. Watahojiwa na PCCB. Hushtuki asubuhi akaunti ina bilioni 1.6, milioni 80 etc. Zimeanguka kutoka juu ya mti. Huo ndo utangulizi.
--Tulitaka kufanya uchunguzi sisi wenyewe na mamlaka zetu na taarifa zimeshakuja, tunazifanyia kazi. Kuna vitu vimetokea, kuna vilivyofanyika nje na taarifa hazikuja na sasa tunalaumiana, hivyo tunafanya uchunguzi na wote waliohusuka tunawahoji na mahakama kuu ipo kesi ya PAP kumiliki hisa za IPTL, ipo kesi ya uhalali wa PAP kupokea pesa za IPTL. Hatutaki kuwaingilia ila sisi tutafanya uchunguzi wetu kwa ajili ya taarifa zetu. Tuwe na uhakika hizi hisa zimeuzwa kwa bei gani, tunataka kujiridhisha kwa sababu ipo kodi ya serikali(capital gain) na inalipwa na alieuza na sio alieuziwa. Kodi hulipwa na aliepata na sio aliepoteza (Alienunua).
--Fedha zilizotoka imelipwa PAP, akitokea mtu ana madai, serikali mnaikinga vipi. Ingetokea mtu ana madai yoyote angepelekwa PAP kulingana na makubaliano. Kukawa kuna hoja kuwa hata PAP umiliki wake wa hisa 70% unatia mashaka kutoka Mechmar, lakini waliziuza kwanza kwa kampuni ya Uingereza ambayo yenyewe ndo ikaziuza PAP. Kampuni ilikua chini ya ufilisi na kwa mujibu wa taratibu huwezi kuuza ukiwa chini ya ufilisi, kwa mujibu wa taarifa sio kweli.
--Kwa upande wa kodi ya serikali ambazo hazikulipwa, AG alipoulizwa alisema hakuna kodi iliyochelewa kulipwa. Mgogoro ni baina ya IPTL na TANESCO havyo uamuzi wa standard charted haukuweza kuingia, kwa vile haikuhusishwa, ilienda kuzuia maamuzi hayo.
--Kabla ya mzozo wa ukokotoaji TANESCO ilikuwa inailipa ITPL Moja kwa moja. Lakini hata ulipotokea mzozo bado IPTL haikuacha kupeleka madai na Tanesco haikuacha kulipa. Kuwepo kwa akaunti ya escrow haibadili mwenye fedha yake.
--Nilipokutana na mwanasheria mkuu, alisema hakukosea katika ushauri wake na wala mahakama haikufanya makosa, na kuhusu ile hasara amesema hakuna hasara yyte iliyopatikana kwa sababu pesa imelipwa kwa mtu halali.
--Jambo moja ambalo ni bahati mbaya, ilijengeka dhana kuwa akaunti kufungwa ni jambo lililoanzishwa na maafisa wa serikali kwa manufaa yao binafsi.
--Na hata TANESCO alipewa ushauri huo huo, uamuzi ule umetiliwa shaka na kuonekana haukuwa sahihi na umeitia hasara nchi. Ukaibua hisia na ni kwa sababu nzuri tu kwamba si bure na iko namna kama ya rushwa na watu kunufaika binafsi. Mara kuna watu wameenda benki na kubeba pesa kwenye sandarusi, lumbesa na mengineyo.
--Mfilisi aliagizwa kuhamisha kwa PAP kutoka IPTL ikiwemo Akaunti ya Escrow, ilizua mjadala mkali. Wizara ya nishati ilimwandikia mwanasheria mkuu kuomba ushauri, Mwanasheria akasema lipeni, uamuzi uko sawa na hauna matatizo na benki kuu wakauliza maswali hayo hayo na majibu yakawa yaleyale. Kuzingatia ushauri huo akaunti ikafungwa na pesa kukabidhiwa PAP. Mjadala ukaendelea bunguni na kwenye mablogu.
--CAG aliwaelekeza TANESCO kuacha kuhesabu pesa walizolipa kwenye akaunti ya escrow kama pesa zao, pesa hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya TANESCO(Asset). Mahakama kuu ya Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri la maombi ya VIP, kusimamisha mchakato wa ufilisi wa IPTL na mahakama ikakubali.
--Kama katika fedha hizo ipo kodi ya serikali, kwa mujibu kulikua na kodi ya ongezeko la thamani ambayo haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini ulikua bilioni 21 na ushee, TRA imepeleka madai yake kwa PAP.
--Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya TANESCO yakakubali ya tozo kupunguzwa, kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za TANESCO ambazo lazima zirudi kwa kiasi kilichopunguzwa. Bahati mbaya miaka saba baadae halikuwa limefanyika.
--Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, mdhibiti wa hesabu alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL, Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikua wanalipa moja kwa moja lakini baada ya mzozo walikubaliana kwanza waziweke BoT.
--Akaunti ikafunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka tozo ya uwekezaji, zinahifadhiwa ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao lakini kabla ya hapo TANESCO walikua wanalipa moja kwa moja.
--Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL
Nianze kuelezea ya Escrow ni kitu gani, ni tofauti kidogo na akauti zetu tatu tulizozizoea, na akauti maalumu na kazi maalumu pia ikiisha na yenyewe inafungwa, inasimamia na wakala na wakala pia anajukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.

--Kwa mujibu wa mkataba, TANESCO isipolipa inatozwa riba ya 2%, kwa mujibu wa taarifa akaunti ilikua na 202.9 bilioni na sio 309.7, hizi zilipaswa kuwepo endapo TANESCO ingelipa zote kwa wakati.
--Masharti ilikuwa kampuni ya IPTL itaendelea kupeleka madai yake TANESCO ya tozo ya uwekezaji na TANESCO itaendelea kulipa lakini yataenda escrow akaunti badala ya IPTL lakini ya umeme yaliendelea kwenda IPTL na ilifunguliwa 2006 na mpaka kesi kuamuliwa 2013 wakati IPTL inachukuliwa na PAP walikua hawajamalizana. (They decided to manage the crisis rather than resolve it)
--TANESCO na IPTL walikubaliana kuanzisha Akaunti ya Tegeta Escrow benki kuu na kuingia mkataba, wizara ya madini kwa niaba ya TANESCO na IPTL na benki kuu kama wakala.
--Rais Kikwete anaelezea kuhusu mgogoro kati ya Tanesco na IPTL mpaka kupelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya Escrow
--Aeleza kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa naye aliagizwa na serikali kufuatilia mihamala ya Escrow na kuchukua hatua stahiki.
--Aaanza kuelezea uamuzi wa Serikali kumtaka CAG kufanya uchunguzi kuhusu akaunti ya Escrow na taarifa kupelekwa bungeni.
--Asema amelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa wale wote waliochangia vurugu katika uchaguzi huo.
--Aelezea furaha yake kuhusu uamuzi wa Mhe. Wassira kuwachukulia hatua wote waliochangia kasoro za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwemo baadhi ya watendaji kufukuzwa kazi huku wengine wakishushwa vyeo.
--Aongelea kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
--Mhe Kikwete aanza kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa zawadi ya ujenzi wa maabara pamoja na kumtakia heri kuhusu afya yake.
--Rais Kikwete ameanza kuongea na wazee wa Mkoa wa Dar katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo Watanzania wanataraji atoe mwongozo kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Qatar, Bw. Yusuf Ahmad Al Hammadi wakati alipotembelea eneo inapojengwa bandari hiyo kubwa na yakisasa akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 22, 2014. (picha na fisi ya Waziri Mkuu)

Monday, December 22, 2014

HATIMAYE diva wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa kali ya mwaka kwa kudai kuwa baada ya kutengana na mzazi mwezake sasa hapati tabu tena kwani mama yake mzazi amechukua nafasi hiyo na anampa mapenzi ya dhati ambayo hajawahi kupewa na mwanaume yeyote.
 
KATIKA hali isiyo ya kawaida, nyumba ya mkazi wa Kata ya Nyasho Manispaa ya Musoma, David Obambo, imeungua moto mara tatu ndani ya mwezi mmoja na kuwashangaza watu.

Temeke ni moja kati ya wilaya tatu zinazounda Jiji la Dar es Salaam. Pia ni jimbo la uchaguzi linaloongozwa na Mheshimiwa Abbas Mtemvu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).Temeke inapatikana Kusini mwa Jiji la Dar es Salaam ambapo kwa upande wa Mashariki, kuna Bahari ya Hindi, Kusini inapakana na Wilaya ya Mkuranga na Kaskazini na Magharibi inapakana na Wilaya ya Ilala.

WIKI iliyopita tuliishia pale ambapo staa wa Bongo Fleva, Diamond aliachia video yake ya Number One katika uzinduzi usiyo na kiingilio alioufanya ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo pia alimzawadia gari, aliyekuwa mwanamuziki nguli nchini, marehemu Muhidin Maalim Gurumo.
Wiki hii tunaendelea ambapo katika kuanika maisha yake, Diamond anasema:

Nyinyiga Raphael (27) ni kijana, mkazi wa Yombo Machimbo wilaya ya Temeke ambaye ndoto zake za kuendelea na masomo zilikatika baada ya kupatwa na maradhi ambayo yanamtesa kwa kipindi cha miaka saba sasa bila kutembea kwa miguu kama ilivyokuwa awali.

DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kigogo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Richard Chengula wiki iliyopita alipata wakati mgumu, baada ya kunusurika kupigwa na wananchi wake, kwa kile kilichodaiwa kuzuia shughuli za maendeleo.

WAKATI Wakristo kote nchini wakijiandaa kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, keshokutwa Alhamisi, baadhi ya familia zipo kwenye majonzi mazito kufuatia kuondokewa na ndugu zao, Uwazi lina kisa cha kuumiza.
angalia hapa......

Sunday, December 21, 2014

Kimenuka! Baada ya kuwepo kwa utata mkubwa juu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya Bongo, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, inadaiwa kwamba waliohusika na kifo chake sasa wanasakwa kila kona.

STAA wa filamu Bongo ambaye miezi michache iliyopita alifunga pingu za maisha na mwanaume mwenye asili ya Denmark, Lucy Komba amekwea pipa kuelekea nchini humo kwenda kuishi na mumewe sambamba na kumpelekea mwanaye amlee.

Ni aibu iliyoje! Tabia ya wanawake kujiuza kwa kisingizio cha kusaka fedha kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi imewatokea puani wanawake zaidi ya kumi akiwemo mke wa mtu baada ya kunaswa mawindoni na kutiwa nguvuni.

STAA wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema anakumbuka fadhila za marehemu Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ ndiyo maana amejitoa kwa hali na mali katika msiba wake kwani anawaonea huruma watoto wake ambao aliishi nao kama kaka yao enzi za marehemu alipokuwa na uhusiano na mdau wa Muziki wa Dansi Bongo, Fikiri Madinda.

Vunja ukimya! Kwa mara ya kwanza, mama mzazi wa mwanamitindo na mkurugenzi wa brand ya urembo ya Kidoti, Jokate Mwegelo, Benadertha Ndunguru amemfungukia mwanaye baada ya kuingia ubia na Kampuni ya Rainbow Shell Craft ya nchini China inayomuingizia mabilioni ya fedha.

STAA wa filamu za Kibongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’  ameamua kuhama jiji la Dar kwa nia ya kumkimbia Bob Juniour ambaye hakuthamini penzi lake.
Staa wa filamu za Kibongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ akipozi.
Akizungumza na waandishi wetu, Sabby alisema kuwa ameona Bob Junior  hamthamini ndiyo maana ameamua kukimbia na kuelekea nchini Kenya akaendelee na maisha yake kwani anao uwezo wa kukaa ‘single’ na kufanya maendeleo.

WAKATI kila mtu akiamini mwalimu wake wa lugha ya Kiingereza ni Wema Sepetu ‘Madam’ staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kudai aliyemfundisha lugha hiyo ni aliyekuwa mpenzi wake, Peniel Mungilwa‘Diamond aliwataka watu wote waliokuwa wakiamini Wema ndiye mwalimu wake wa ung’eng’e wafute imani hiyo kwani Penny ndiye mpango mzima.

Thursday, December 18, 2014

Amekwenda mapema mno! Siku ya Desemba 17, mwaka huu haikuwa poa hata kidogo kwenye tasnia ya muziki wa dansi Bongo katika kipengele cha unenguaji.

Ijumaa: Umekuwa ukitajwa kuwa wewe ni msanii wa kike unayeongoza kwa kubadilisha mabwana kila kukicha, hili likoje?
Baby Madaha: Ukweli hiyo huwa inatokea tu na huwa sipendi kusumbuliwa na mwanaume, nikiona ananizingua nammwaga. Hata hivyo, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza, nafanya kazi, mapenzi pembeni.
Ijumaa: Unadhani kwa nini umekuwa ukiingia kwenye uhusiano kisha kutoswa, ni umachepele wako au kitu gani?

Mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' (wa tatu kulia) akipata chakula cha usiku na wageni wake wakiongozwa na staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' (katikati) usiku wa kuamkia leo nchini Uganda.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, akiongea na wanahabari hivi punde ndani ya Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam amesema haoni sababu ya kujiuzulu kutokana na sakata la akaunti ya Escrow.
Aongeza kuwa watu wanaona suala la kujiuzulu kama fasheni ila yeye hayupo katika fasheni hiyo.

ALIYEKUWA mnenguaji na mwimbaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda aliyefariki jana asubuhi, atazikwa kesho mchana badala ya leo kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeteuliwa hivi karibuni, Daud Felix Ntibenda alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani humo.

Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Uganda jana.

Mtoto Raphael Barnaba (4) kutoka mkoani Mbeya anayetibiwa miguu katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam, akipokea kwa furaha zawadi ya matunda kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Vodacom kitengo cha Rasilimali Watu, Alice Lewis (katikati) wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na kuwagawia matunda kama sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom chini ya Vodacom Foundation wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka. Akitazama ni mama wa mtoto huyo (wa kwanza kushoto).

Wanajeshi hao wakiwa mbele ya Mahakama ya Kijeshi jijini Abuja nchini Nigeria.
Mahakama ya Kijeshi nchini Nigeria imewahukumu adhabu ya vifo wanajeshi wake 54 waliokataa kupambana na wapiganaji wa Kundi la Boko Haram.

Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.

Wednesday, December 17, 2014

MSANII wa filamu Bongo, Salim Omary  ‘Slim’  hivi karibuni alitoa kali ya mwaka baada ya kufunga sambusa ukumbini na kuondoka nazo kwa kile alichodai hana wa kumpikia.
Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO