
Kaka mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Nicholaus kwa kushirikiana
na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, amesimamia
fumanizi la dada’ke ambaye ni denti wa sekondari moja jijini Dar (majina
yanahifadhiwa kwa sababu maalum) ambapo alimfumania chumbani na njemba
mmoja sharobaro aliyetajwa kwa jina la Abuu Ally, mkazi wa
Mbagala-Charambe, Dar.


OFM ikiwa kazini, ilipokea malalamiko
kutoka kwa Nicholaus aliyedai kwamba amekuwa akiumizwa na taarifa kwamba
kila ikifika saa 2: 00 usiku kuna mwanaume amekuwa akijipenyeza na
kuingia chumbani kulala na mdogo wake wa kike kisha kuchomoka alfajiri.
Nicholaus alisema kuwa mara nyingi vitendo
hivyo hufanyika wikiendi ambapo katika kuhangaika kumnasa anayemharibu
mdogo wake aliwataarifu OFM ambao waliingia mzigoni na kuweka mtego
uliomnasa sharobaro huyo.

OFM hawakuwa wenyewe kwani walimtaarifu
Mjumbe wa Mtaa wa Maji-Matitu, Hawa Ally kuwa wana kazi eneo lake hivyo
akatoa ushirikiano uliofanikisha kumnasa Abuu.
Ama kweli za mwizi arobaini! Saa 5:11 usiku, jamaa huyo aliingia chumbani kwa denti huyo na kuanza makeke yake akimfanyia binti huyo mavituzi.
Ama kweli za mwizi arobaini! Saa 5:11 usiku, jamaa huyo aliingia chumbani kwa denti huyo na kuanza makeke yake akimfanyia binti huyo mavituzi.

Baada ya kukiri kosa mbele ya kiongozi huyo wa serikali za mtaa, pande zote zilikubali kusuluhishwa ambapo Abuu alikubali kulipa faini ya shilingi laki moja na kupewa muda wa siku moja kutekeleza adhabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment