
STAA mwenye shepu ya aina yake ndani ya Bongo Movies, Tamrina Poshi ‘Amanda’ ameibuka na kusema kuwa siku ikifika atarejea kwa Mwenyezi Mungu lakini kwa sasa bado anakula ujana.
ujana.
Akipiga stori na Ijumaa Wikienda, Amanda
alisema kwa sasa umri wake unamruhusu kula ujana kwa mambo ya starehe
kama kuvaa mavazi ya kuacha mwili wake nusu utupu kwa sababu muda wa
kurejea kwa Mungu bado haujafika.

“Jamani niacheni na mavazi yangu, ukifika
muda nitarejea naona mnanisema sana, kama wewe Mungu amekujalia kusali,
mshukuru mimi muda huo bado haujafika,” alisema Amanda ambaye wakati huo
alikuwa ametupia kivazi kilichomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake
hasa tumboni.
0 comments:
Post a Comment