
Kimenuka! Baada ya kuwepo kwa utata mkubwa juu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya Bongo, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, inadaiwa kwamba waliohusika na kifo chake sasa wanasakwa kila kona.

Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake.
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni,
Dar, zilidai kwamba jeshi hilo ndilo lililozuia mazishi ya staa huyo
hadi mwili ufanyiwe uchunguzi.“Ukweli ni kwamba majibu ya kilichomuua
hayajawekwa wazi lakini wote waliokuwa naye dakika za mwisho wanasakwa
kwani kuna madai mazito kwamba alipewa kitu na watu wasiojulikana.
‘Aisha Madinda’wakati akiwa na Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka.

Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura.
Ili kupata undani wa ishu hiyo, Jumamosi iliyopita Ijumaa Wikienda
lilizungumza na Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura ambaye
alikuwa na haya ya kusema:“Kwanza majibu hayajatoka hivyo ni mapema kuyazungumzia. Madai kwamba kuna mtu mmoja amekamatwa si ya kweli.”
Aisha (35) alizikwa Ijumaa iliyopita huko Kigamboni, Dar, baada ya kukutwa na umauti wa kutatanisha Jumatano ya wiki iliyopita.
0 comments:
Post a Comment