
ACHANA
na watu kibao waliojitokeza mitandaoni na kudai wana undugu na mshindi
wa Shindano la Bigbrother Hotshot (2014), Idris Sultan (21), mwigizaji
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ndiye mtu wa kwanza kabisa kujinadi kuwa na
urafiki na mshindi huyo aliyejinyakulia zawadi ya shilingi milioni 510.

Siku alipotangazwa ushindi, kesho yake
(Jumatatu) Lulu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutupia picha ya zamani
katika mtandao wa Instagram akiwa na Idris na kuacha gumzo kwa wafuasi
wa mtandao huo juu ya ukaribu huo kiasi cha kupiga picha ya pamoja.

Mbali na Lulu, baadaye wasanii wengine walifuata mkumbo huo wa kuweka picha wakiwa na Idris ambazo wengi walikuwa na lengo la kumpongeza mshindi huyo ingawa Wabongo wengi walidai kuwa wanajipendekeza.Katika mazungumzo yake na mwanahabari wetu, mbali na mipango mingine, Idris amepanga kuwekeza sehemu ya fedha zake katika soko la filamu Bongo.
0 comments:
Post a Comment