
MSANII wa filamu Bongo, Salim Omary ‘Slim’ hivi karibuni alitoa kali ya mwaka baada ya kufunga sambusa ukumbini na kuondoka nazo kwa kile alichodai hana wa kumpikia.
Baadhi ya wasanii wenzake waliokuwa ukumbini hapo walionekana wakimshangaa na kumuuliza kulikoni kuchukua sambusa za shughuli na kuzifungasha kwenye pochi ya msanii mwenzake, Jack Pentzel ‘Jack Chuz’.
“Kwa sasa sina mke baada ya kuachana naye hivyo naishi hivi, sambusa hizi zitanisaidia asubuhi kunywa chai,” alisikika Slim akiwajibu wasanii wenzake.
0 comments:
Post a Comment