
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huduma mpya ya
HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia
kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu
32 ndani ya familia na kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo
mahali popote nchini Tanzania kufurahia internet ya 3.75G. kulia ni
Meneja Masoko wa Airtel Home WiFi, Gaurav Dhingra.
Meneja
Masoko wa Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huduma mpya ya
HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia
kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu
32 ndani ya familia na kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo
mahali popote nchini Tanzania kufurahia internet ya 3.75G. Kulia ni
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando na kushoto
ni Ofisa Masoko wa Airtel Tanzania,Ndevonaeli Eliakimu.

Mkutano ukiendelea.
Airtel Tanzania leo imezundia huduma ya kwanza ya kibunifu nchini
ijulikanayo kama “Home WiFi with bundle share” (WiFi ya nyumbani na
kufurushi cha pamoja) itakayowawezesha watanzania na wateja wa Airtel
kupata huduma ya Wi-Fi na kuunganisha zaidi ya vifaa vingine 32
vitakavyotumia WiFi .
Huduma hii vilevile itaunganisha hadi simu 4 za mkononi zilizoko
kokote nchini kwenye akaunti moja na kuwapatia internet ya kasi ya
3.75G. hii inamaanisha kifurushi cha internet kilichopo kwenye kifaa
cha WiFI ya nyumbani sasa kitakuwa na matumizi mawili yaani Wifi ya
nyumbani na internet kwenye simu za mkononi pindi mteja akiwa nje ya
nyumbani
kwa sasa wanafamilia na watumiaji wa intenet Tanzania hawana haja
ya kununua vifurushi vya intenet kwa kila simu , kompyuta, Television au
vifaa vyovyote vinavyoweza kuunganishwa na internet na badala yake
watakachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi kwenye WiFi ya nyumbani na
kuwawezesha kila aliyeunganishwa na kifaa hicho kupata kifurushi chake
kulingana na gawiwo alilowekea na hivyo kutumia kifurushi kimoja
ili kujipatia kifaa hichi cha HOME WiFi unaweza ukalipia : shilingi
195,000/- na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha 40 GB kwa mwenzi au
unaweza kulipia shilingi 250,000/- na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha
120 GB kwa mienzi mitatu, Aina zote mbili za ofa zinatoa huduma ya
kutumia kifurushi kimoja na kuunganisha wanafamilia wanne wenye simu za
mkononi ya malipo ya awali (prepaid line)
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja masoko na bidhaa
hii wa Airtel Bw, Guarav Dhingra alisema” Dunia inabadilika na kukua
kwa kasi ndivyo ilivyo kwa matumizi ya internet, kwa sasa internet si
kwa ajili ya baba na mama, bali ni muhimu kwa familia nzima ikiwa ni
pamoja na watoto kwaajii ya burudani, masomo, na nyingine nyingi.
Ongezeko kubwa la simu za kisasa, komputa ndogo, Television za Kisasa,
saa za kisasa, tablet katika nyumba zetu ni ushahidi tosha wa hili.
Wakati ongezeko na upatikanaji wa vifaa hivi ukiwa rahisi, njia za
kuunganiswa na huduma za internet zinazidi kuwa ngumu kwa wateja,
kwani inamgharimu mteja kuwa na simcard kwa kila kifaa, na kila simcard
inabidi kusajiliwa na kuwekewa muda wa maongezi wakutosha , kisha
kuingiza namba maalumu na kuchangua kirufushi na ndipo kuanza matumizi.
Airtel kwa kuona hii changamoto imekuja na huduma ya WiFi ambapo
sasa unaweza kuunganisha vifaa hivi vyote kupitia kifaa cha WiFi cha
nyumbani na kupata intenet ya kasi bila kuhitaji simcard yoyote ya
ziada. Na tumewawezesha wanafamilia kuweza kuongeza kifurushi cha
intenet kwa kupiga *148*20# na kuunganishwa na kifurushi kimoja
Tunaamini familia nyingi zaidi nchini Tanzania watafurahia na
kutumia huduma hii ya pekee toka Airtel na hivyo kutuamasisha kuongeza
huduma nyingi za kibunifu za internet” aliongeza Guarav Dhingra
Huduma hii inapatikana kwa kupiga 0784104800 ambapo utaweka oda
yako kwajili ya kupata kifaa hiki cha WiFi ya nyumbani, na kisha
Airtel itakuletea mahali ulipo na kukunganisha na huduma hii.
0 comments:
Post a Comment