
JAMAA
wawili, mmoja fundi umeme, Rashid Balazi na Juma Bushiri wanadaiwa
kunusurika kifo baada ya kutekwa na kusulubiwa nyumbani kwa msanii wa
sinema za Kibongo, Wema Sepetu wakituhumiwa kukwapua simu ya bei mbaya
ya mpambe wa mwanadada huyo, Petit Man, Amani limeichimba kwa kina.
Wakielezea mkasa huo wa kutisha uliojiri mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, manusura hao walisema siku ya tukio waliitwa nyumbani kwa Wema na mdogo wake aitwaye Bite kwa ajili ya kutengeneza mota ya kusukuma maji.Walisema walifika nyumbani hapo na kuangalia mota hiyo ambapo waligundua kwamba haikuwa na tatizo bali mushkeli ilikuwa kwenye bomba la maji.
WAOMBA FEDHA YA MANUNUZI
Walisimulia kwamba, baada ya kugundua hilo waliomba fedha kwa Bite kwa ajili ya kwenda kununua bomba, wakapewa shilingi elfu arobaini.“Lakini kabla hatujafika kunakouzwa mabomba tulipigiwa simu na Bite kwamba tunatakiwa kurudi kwa kuwa kuna tatizo.
Walisimulia kwamba, baada ya kugundua hilo waliomba fedha kwa Bite kwa ajili ya kwenda kununua bomba, wakapewa shilingi elfu arobaini.“Lakini kabla hatujafika kunakouzwa mabomba tulipigiwa simu na Bite kwamba tunatakiwa kurudi kwa kuwa kuna tatizo.
“Tulipoona tumevaa msala wa uongo tulimwambia atupeleke polisi, akasema atawaita makamanda wake ambao ni ‘mbwa mwitu’ waje watuoneshe kazi. Lakini kabla ya kuwaita makamanda wake, alimwita mganga wa kienyeji. “Mganga alifika akaangalia kwa darubini zake akasema simu hatujaiba sisi, lakini Petit Man hakutaka kumwelewa.
“Wakati huo alikuwa bado ametufungia ndani tusitoke, ghafla wakafika hao makamanda wake, hatukuwahesabu lakini walikuwa wengi, wakatuteka na kutufunga kabla ya kuanza kutusulubisha wakidai wao ni ‘mbwa mwitu’. Jamaa walitupiga kipigo cha mbwa mwizi....”
SILAHA ZATUMIKA
“Kama hiyo haitoshi, Petit Man aliwaita mabaunsa wawili ambao walitutesa na kutuvua nguo tukabaki kama tulivyozaliwa.
PETIT MAN MBARONI
“Kipigo kilipozidi majirani walisikia kelele na kuja kuchungulia ambapo walikimbilia kwa mjumbe wa nyumba kumi na kumpa taarifa, yeye akaja kutuokoa na kutupeleka polisi huku wakati huo difenda la polisi nalo likawa limeshafika na kumtia mbaroni Petit Man na baadhi ya watesaji hao na kwenda kuwasweka mbaroni kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ lakini wengine walikimbia.”
Baadhi ya majeraha aliyoyapata Juma Bushiri.
WEMA ATOKA“Kipigo kilipozidi majirani walisikia kelele na kuja kuchungulia ambapo walikimbilia kwa mjumbe wa nyumba kumi na kumpa taarifa, yeye akaja kutuokoa na kutupeleka polisi huku wakati huo difenda la polisi nalo likawa limeshafika na kumtia mbaroni Petit Man na baadhi ya watesaji hao na kwenda kuwasweka mbaroni kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ lakini wengine walikimbia.”
“Wakati zogo hilo linaanza, Wema alitoka na kumwambia Petit wawahi uwanja wa ndege (Julius Nyerere, Dar) kwani walikuwa na safari (walikuwa wanakwenda nchini Ghana).
“Wema na Petit Man waliondoka na kuamuru kwamba tuwasubiri hapohapo tusiondoke.”
KIPIGO SAA 6:00 MCHANA HADI 9:00 ALASIRI
“Walipofika uwanja wa ndege wakawa wamechelewa ndege, Wema hakurudi nyumbani ila Petit Man alirudi ndipo tukaanza kupigwa kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 alasiri,” walieleza jamaa hao wakiwa hoi kwa kipigo cha shetani.
MAJERAHA
Katika tukio hilo, Juma alipata majeraha kibao mwilini ambapo anatembea na mkongojo huku Rashid akiwa amechanwa na kisu mgongoni, mguuni na mbavu moja ikiwa imepata ufa na wote hao walipelekwa kwenye Hospitali ya Sinza-Palestina, Dar.Baadaye Rashid alihamishiwa Mwananyamala kufuatia hali yake kuwa mbaya.

Siku ya kwanza Petit Man alilala kituoni ambapo kesho yake Wema alitinga, naye akatupwa lupango kisha kuchukuliwa maelezo kabla ya baadaye wote kuachiwa ambapo Petit Man alitoka kwa dhamana.
Hata hivyo, washitakiwa hao na walalamikaji walitakiwa kuripoti kituoni hapo Jumatatu iliyopita lakini walalamikiwa walikiuka amri ya polisi, hawakuonekana kwa madai kwamba wamesafiri kikazi kwenda nchini Ghana.
SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI
Kwa mujibu ya shitaka lililofunguliwa kituoni hapo, Petit Man anakabiliwa na tuhuma za kudhuru mwili katika jalada la kesi namba KJN/RB/11250/2014 na KJN/RB/11220/2014 -SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.

MJUMBE AKIRI
Naye mjumbe wa eneo la tukio, Muharami Seif alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukiri kuwaokoa jamaa hao wakiwa katika hali mbaya baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani hivyo Petit Man na Wema wanasubiriwa watue Bongo kukabiliana na mkono wa sheria.
0 comments:
Post a Comment