Thursday, December 18, 2014



Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeteuliwa hivi karibuni, Daud Felix Ntibenda alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani humo.

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati Mkuu wa Mkoa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza mazungumzo yao.

0 comments:

Post a Comment

Design by hons.CISKO | Blogger Theme by CISKO