KIFO
cha utata cha mnenguaji nyota Bongo, Mwanaisha Mbegu maarufu kama Aisha
Madinda, kimemuibua Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ wa FM Academia,
aliyewataka wenzake kuwa makini ili kutojiingiza katika utumiaji wa
madawa ya kulevya.
Akistorisha na paparazi wetu, Queen Suzy alisema ameumizwa sana na
kifo hicho kwani ameacha pengo kubwa kutokana na unenguaji wake mzuri,
huku chanzo cha kifo chake kikiwa hakifahamiki sawasawa.
“Nawasihi wanenguaji wenzangu na wanamuziki wote, tusidanganyike
kuingia kwenye vishawishi vya matumizi ya madawa ya kulevya, maana mfano
Aisha alikuwa mzuri kweli kwenye kazi, lakini alipojiingiza kwenye unga
kiwango chake kikashuka sana,” alisema Queen Suzy.